728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, March 29, 2016

    UWANJA WA NOU CAMP KUBADILISHWA JINA

    Barcelona,Hispania.

    Wakuu wa klabu ya FC Barcelona wakiongozwa na Rais Josep Maria Bartomeu leo jumanne watakutana kupitisha mpango wa kuubadili jina uwanja wa Nou Camp na kuuita Johan Cruyff ikiwa ni ishara ya kumuenzi gwiji wake huyo aliyefariki dunia wiki iliyopita kwa maradhi ya Kansa.

    Mpango huo wa kuubidili jina uwanja wa Nou Camp umekuja zikiwa ni siku chache tu tangu Uholanzi itangaze kuubadili jina uwanja wake wa taifa wa Amsterdam Arena na kuuita Johan Cruyff.

    Kwa mujibu wa Radio Catalunya sehemu kubwa ya mashabiki wa FC Barcelona wanauunga mkono mpango huo wa kuubadili jina uwanja wa Nou Camp kwa ajili ya kuuenzi mchango wa Cruyff kama mchezaji na kocha.

    Uwanja wa Nou Camp ulianza kutumiwa na FC Barcelona mwaka 1957 ukiwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 99, 351.

    MAFANIKIO YA CRUYFF AKIWA NA FC BARCELONA

    Akiwa kama mchezaji Cruyff aliiongoza FC Barcelona kutwaa taji la La Liga mwaka1974,Copa del Rey mwaka 1978.

    Akiwa kama kocha Cruyff aliiongoza FC Barcelona kutwaa mataji manne ya La Liga,mataji matatu ya Super Cup ya Hispania,taji moja la Copa del Rey,European Cup, Uefa Super Cup na kombe la washindi.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: UWANJA WA NOU CAMP KUBADILISHWA JINA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top