728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, March 23, 2016

    COURTOIS:CHELSEA ILIKUWA SAHIHI KUMTIMUA JOSE MOURINHO

    Brussels,Ubelgiji.

    Mlinda mlango wa Chelsea Thibaut Courtois amesema kuwa klabu hiyo ilikuwa sahihi kumtimua kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Mreno Jose Mourinho hapo mwezi Disemba mwaka jana na nafasi yake kuchukuliwa na Guus Hiddink.

    Courtois,22 akiongea na kituo cha RTBF cha nyumbani kwao Ubelgiji ambako amekwenda kukitumikia kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo amesema maandalizi mabaya ya mwanzo wa msimu chini ya kocha Jose Mourinho ndiyo yaliyochangia kufanya vibaya kwa klabu ya Chelsea.

    Amesema "Ni ngumu kueleza ni kwanini msimu huu umekuwa mbaya sana kwetu kiasi cha kukatisha tamaa.Labda ni matokeo ya jinsi maandalizi ya msimu huu yalivyokuwa,yalikuwa mafupi sana.

    Tulianza maandalizi Julai 16 na siku sita baadae tukacheza mchezo wa kwanza dhidi ya New York Red Bulls.Hatukuwa vizuri kimwili na matokeo yake tukafungwa na Arsenal katika mchezo wa ngao ya jamii na baada ya hapo kukaendelea kuvurunda.

    Tulihitaji Kocha mpya aje kuweka mambo sawa,sina shaka juu ya hilo.Tulitoka sare michezo mingi huku tukifungwa magoli rahisi rahisi".



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COURTOIS:CHELSEA ILIKUWA SAHIHI KUMTIMUA JOSE MOURINHO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top