Cluj,Romania.
Mchezo wa soka umeendelea kutumiwa kama jukwaa la kufikisha jumbe mbalimbali kwa jamii katika kila pande za dunia.
Jumbe hizo huwa ni maalumu kwa ajili ya kuhamasisha/kuonya ama kutoa taarifa fulani kwa jamii lengwa.
Siku ya jumapili katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki kati ya Romania na Hispania historia nyingine iliandikwa.
Katika mchezo huo uliopigwa Cluj na kuisha kwa sare ya 0-0 wachezaji wa Romania walivaa jezi za mazoezi zenye maswali mbalimbali ya hisabati ili kuhamasisha watoto wa taifa hilo kupenda somo hilo na kujifunza.Hisabati ni jana nchini Romania.
Nchi ya Romania inakabiliwa na tatizo kubwa la utoro mashuleni takribani asilimia 18 ya watoto wa nchi hiyo wameacha shule kwa sababu mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment