BY GASCOIGNE BRIAN.
Muda mwingine tunatakiwa kukubaliana na hali iliyopo ili dunia iweze kujizungusha katika mhimili wake na wote tunajaribu kukimbizana na muda ili tufike pale panapostahili.
Ni muda ambao Leichester city anatupa kile kilicho bora kutoka kwa Mahrez ni ubora ulioje!!!..ni kipindi ambacho Wenger bado anajaribu kuiaminisha dunia kuwa ataweza kuvaa medali ya Barclays chini ya Oliver Giroud huku Dimitri Payet akiwa West ham.
Mwanaharakati mmoja mchini marekani Malcolm x aliwahi kusema. IF YOU HAVE NO CRITICS YOU WILL LIKELY HAVE NO SUCCESS (KAMA HUNA WAKOSOAJI HAUTAKUWA NA UWEZEKANO WA KUFANIKIWA).Hata Van Gaal yakumbuke sana maneno ya Malcolm x huenda ukaamka kutoka kwenye usingizi mzito uliolala,kuamini ulichonacho ni bora sana kuliko kusubiri kijacho maana huwezi jua kitakuja kuwa na ubora kiasi gani.
Frolent Dimitri Payet ni bidhaa nyingine ambayo inaelekea kuwa lulu katika dirisha la usajili kipindi kijacho,ndio muda ambao pesa za waarabu zitakuwa bize kutafuta ubora wa miguu yako yenye thamani ya Bugatti Veyron ikiambatana na sura ya upole ndani yake.
Niliwahi kusema hapo nyuma kuwa usawa wa dunia isiyo na usawa inakaribia kupatikana,ndio maana Leichester yupo
pale alipo pamoja na spurs huku West ham na Payet wao nao wakikaribia kuisogelea usawa wa dunia.Hata Guss Hiddink
anatamani sana kuwa alipo Leichester city ila ukomavu [MATULITY] ya wachezaji wake umeishia pale walipo.
Sina shaka sana na Liverpool pale walipo naimani watakuja kuwa na msimu mzuri msimu ujao kama akiweza kufanya usajili mzuri katika
kikosi chake hasa katika maeneo muhimu.Slaven Bilic najua hatuamini sana ubora wako,ila tunaelewa kile unachoendelea
kutupa kilicho bora na kinachostahili kwa wakati mmoja.Umeleta kipaji halisi katika ligi yetu pendwa,anayetupa utamu kila siku za wikiendi pale nchini Uingereza.
Wakati mwingine safari ya mshindi huwa na mizunguko mingi
mpaka kufika pale panapostahili,naiona safari ya Payet huku gari yake ya Bugatti ikiwa karibu kufika nyumbani kwake.Ufalme
wetu wa Big 4 umekwisha maana usawa unakaribia kupatikana wa dunia iliyokosa usawa,hata rafiki yangu Shaffih dauda anajua hili.
Ni muda ambao ukomavu wa Wenger na uzoefu wake ulitakiwa kuonekana hapa,lakini kutokana na kushindwa kuamini
maneno ya Malcolm x ndio maana yupo pale alipo.
Akili ya mwanadamu wakati mwingine hutegema na matarajio ya kile alichonacho kwa kuamini kinaweza kumfikisha au kumpeleka mahala salama hata Aston villa wanalijua hili ndio maana hawapotezi muda mwingi kupambana pale walipo maana kwa
udhaifu wa timu yao washajua wapi wanastahili kwenda,bado nawaza sana ubora wa Mauricio Pochettino uliozungukwa na ubora wa kikosi chake ni bidhaa nyingine adimu itakayokuja kuwa lulu katika dirisha la usajili kwa upande wa makocha.
Manuel Pellegrini tatizo unaishi kwa matumaini wakati walishakuzika mapema,kivuli chako ndio kinaendelea tuu kubaki
pale kilipo ila hata wewe akili yako tayari umeshaipeleka kwa
mkeo kipenzi mwanamama Carola Pucci ambae ndio kipenzi cha kweli juu yako.
Najua safari ya Guardiola ndio imetibua hali hewa kwako ila ubora wa Kun Aguero unaweza kukupa heshima ya kuweza kufika mbali katika Champions league.Dimitri payet
usiku wa jumatano lenye baridi kali katikati ya uwanja ukikatiza
kwa ubora wa hali ya juu ukiweza kufanya yako mbele ya mashabiki zaidi ya 50,000 katika Champions league wakikushangili huku Bugatti veyron ikiwa imepaki nje ikisubiri iweze kukupeleka nyumbani na sura yako yenye tabasamu la upole nilionekana mbele ya macho yako.
Naisubili sana safari
yako ya matumaini ya kufika pale panapostahili maana harufu ya miguu yako inanionyesha hivi,karibu tena katika ufalme wetu.
0 comments:
Post a Comment