Accra,Ghana.
Ghana,Nigeria na Cameroon jana jumamosi zilifanikiwa kukata tiketi ya kuingia katika kinyang'anyiro kombe la dunia la mwanawake la wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 baada ya kuibuka na ushindi dhidi ya Morocco,Afrika Kusini na Misri.
Ghana ikiwa nyumbani Accra imeibanjua Morocco kwa mabao 6-0 na kufanikiwa kufuzu kwa jumla ya mabao 10-0 baada ya mchezo wa kwanza kushinda kwa mabao 4-0.
Nigeria wakiwa ugenini Johannesburg wamewatandika wenyeji wao Afrika Kusini bao 1-0.Bao pekee la mchezo huo limefungwa na nahodha Rasheedat Ajibade.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Abuja,Nigeria ilitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 6-0.
Katika mchezo mwingine Cameroon imefanikiwa kufuzu michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kuitambia Misri na kuichapa mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa Cairo.Katika mchezo wa kwanza Cameroon ilishinda 2-1.
0 comments:
Post a Comment