Cordoba,Argentina.
Lionel Messi amefunga goli lake la 50 na kuiongoza Argentina kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Bolivia huko Cordoba katika mchezo mkali wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia la 2018 kwa ukanda wa Amerika Kusini (CONMEBOL).
Messi amefunga goli hilo kwa mkwaju wa penati baada ya walinzi wa Bolivia kufanya madhambi golini kwao.Goli jingine la Argentina limefungwa na Gabriel Mercado.
Ushindi dhidi ya Bolivia umeipandisha Argentina mpaka nafasi ya pili na pointi zake 11 nyuma ya vinara Uruguay na Ecuador wenye pointi 13 baada ya kushuka dimbani mara sita.
Katika michezo mingine Uruguay imeifunga Peru 1-0 kupitia kwa Edinson Cavani,Brazil imetoka sare ya 2-2 na Paraguay,Chile imeichapa Venezuela 4-1 huku Colombia ikiifunga Ecuador 3-1.
0 comments:
Post a Comment