London,Uingereza.
Mlinda mlango Peter Cech ametangaza kuwa atastaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Jamhuri ya watu wa Czech mara baada ya kuisha kwa michuano ijayo ya Ulaya (Euro 2016) inayotarajiwa kupigwa huko Ufaransa baadae mwaka huu.
Cech,33 aliyeanza kuichezea Jamhuri ya watu wa Czech mwaka 2002 amesema muda umefika wa yeye kukaa pembeni na kuwapisha wengine waje kutoa mchango wao huku yeye akielekeza zaidi akili yake katika kuitumikia klabu yake ya Arsenal.
Cech atakumbukwa daima baada ya mwaka 2004 kuisaidia Jamhuri ya watu Czech kutinga hatua ya nusu fainali ya Ulaya iliyochezwa nchini Ureno huku yeye akitangazwa mlinda mlango bora wa michuano hiyo.
.
0 comments:
Post a Comment