Na.Paul Manjale.
Barcelona,Hispania.
Je unajua kuwa Javier Mascherano hajawahi kuifungia FC Barcelona bao lolote tangu ajiunge nayo mwaka 2010 akitokea Liverpool!?
Unadhani hali hii inamuumiza kiungo huyu wa shoka???Sasa sikia hii.Akiongea na chombo kimoja cha habari cha nyumbani kwao Argentina cha TyC Sports Mascherano,31 amefichua kuwa mara kadhaa amekuwa akipata ofa toka kwa Lionel Messi ya kupiga penati pindi zinapotokea ili aondoe gundu la kutofunga lakini amekuwa akikataa kata kata.
Amesema "Mara nyingi Messi amekuwa akinipa mpira nipige penati na mimi nijipatie walau bao moja lakini nimekuwa nikimkatalia.Sipendi kulazimisha vitu ambavyo haviendani na mimi".
Sipendi matokeo yabadili majukumu niliyonayo uwanjani.Mwenye jukumu la kupiga penati acha aendelee"Alisisitiza Mascherano.
Mascherano ambaye mpaka sasa ameichezea FC Barcelona zaidi ya michezo 200 hajafunga bao lolote.Mara ya mwisho Mascherano kufunga bao ilikuwa ni Machi 2008 alipoifungia Liverpool katika ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Reading.
0 comments:
Post a Comment