De 4-Aout,Burkina Faso.
Washambuliaji Emmanuel Okwi na Hamisi Kiiza jana jumamosi usiku walishindwa kuisaidia Uganda na kujikuta wakikubali kichapo cha goli 1-0 toka kwa Burkina Faso katika mchezo wa Kundi D wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON 2017.
Goli pekee la mchezo huo ulipigwa katika dimba la Stade De 4-Aout limefungwa na mshambuliaji Jonathan Pitriopia dakika ya 59 kwa mkwaju wa penati uliotolewa na mwamuzi toka Misri Ghead Grisha baada ya madhambi kutendeka langoni mwa Uganda.
Uganda na Burkina Faso zitarudiana tena siku ya jumanne katika dimba la Nelson Mandela jijini Kampala.
Kikosi cha Uganda Cranes kilikuwa hivi:
Denis Onyango (G.K), Denis Iguma, Joseph Ochaya, Murushid Juuko, Isaac Isinde,Tonny Mawejje, William Luwagga
Kizito, Khalid Aucho/ Hamis Kizza,Farouk Miya, Geofrey Massa, Godfrey Walusimbi/ Emmanuel Okwi.
0 comments:
Post a Comment