Valencia,Hispania.
Valencia imemtupia virago aliyekuwa kocha wake mkuu Muingereza Gary Neville ikiwa ni miezi minne tu tangu ajiunge nayo akichukua nafasi ya Nuno Espirito Santo.
Valencia imefikia hatua ya kumtupia virago Neville baada ya mlinzi huo wa zamani wa Manchester United na England kushinda michezo mitatu pekee kati ya 16 aliyohudumu kama kocha wa Los Che.
Itakumbukwa Neville akiwa kama kocha wa Valencia alishuhudia kikosi chake kikitupwa nje ya michuano ya Ulaya na Olympique Lyon huku kikikung'utwa mabao 7-0 na FC Barcelona katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la Copa del Rey.
Neville anaiacha Valencia ikiwa nafasi ya 16 katika msimamo wa ligi ya La Liga,pointi sita juu ya mstari wa kushuka daraja.
Wakati huohuo Valencia imemtangaza kocha msaidizi wa zamani wa Liverpool Pako Ayestaran kuwa kocha wake mkuu mpaka mwisho wa msimu.
0 comments:
Post a Comment