728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 26, 2016

    BARCA YAISHIKA PABAYA ARSENAL

    Barcelona,Hispania.

    WAMESHIKWA PABAYA!!FC Barcelona imepania kuhakikisha msimu ujao kiungo wa Arsenal Mesut Ozil anatua Nou Camp kuwapikia mabao zaidi Messi,Neymar na Luis Suarez.

    Taarifa kutoka nchini Hispania na kuthibitishwa na gazeti la AS zinadai FC Barcelona imepanga kuwatumia kama chambo nyota wake watatu Arda Turan, Sandro Ramirez na Munir El-Haddary ili kumnasa Ozil aliyetua Arsenal mwaka 2013 akitokea Real Madrid kwa dau la £42.5m.

    Hata hivyo mpango huo unaweza ukapata upinzani mkali toka kwa Real Madrid ambayo iliipa Arsenal sharti la kuipa nafasi ya kwanza kabla ya kuamua kumuuza kwingineko kiungo huyo Mjerumani.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BARCA YAISHIKA PABAYA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top