728x90 AdSpace

Wednesday, March 30, 2016

UJERUMANI YAICHAPA ITALIA BAADA YA KUISHINDWA KWA MIAKA 21

Munich,Ujerumani.

Hatimaye Ujerumani jana jumanne usiku iliondoa gundu la kushindwa kuifunga Italia kwa kipindi cha miaka 21 baada ya kuichapa magoli 4-1 katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa katika dimba la Allianz Arena, 

Ujerumani ambayo ilikuwa haijapata ushindi dhidi ya Italia tangu mwaka 1995 ilijipatia magoli yake kupitia kwa Toni Kroos (24'),Mario Götze (45'),Hector (59') huku Mesut Özil akifunga dakika ya (75') kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya mlinda mlango Gigi Buffon kumwangusha katika eneo la hatari Antonio Rudiger.

Goli la Italia limefungwa na Stephan El Shaarawy dakika ya 83.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: UJERUMANI YAICHAPA ITALIA BAADA YA KUISHINDWA KWA MIAKA 21 Rating: 5 Reviewed By: Unknown