Munich,Ujerumani.
Klabu ya Manchester United imepata pigo baada ya kiungo wake Bastian
Schweinsteiger kuripotiwa kuwa atakosa michezo yote iliyobakia ya ligi kuu nchini England baada ya kuumia goti.
Schweinsteiger,31aliumia goti hilo siku ya jana jumanne wakati akifanya mazoezi na wachezaji wenzake katika kambi ya timu ya taifa ya Ujerumani inayotarajiwa kucheza michezo ya kirafiki ya kujipima nguvu dhidi ya England na Italia.
Kwa mujibu wa vipimo vya MRI scan vilivyofanywa na daktari Hans-Wilhelm Müller-Wohlfahrt ni kuwa Schweinsteiger ameumiza vibaya goti lake na hivyo atakuwa nje ya dimba kwa kipindi kirefu na kuyaweka mashakani majaaliwa ya nyota huyo kucheza michuano ijayo ya Ulaya inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Juni huko Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment