Barcelona,Hispania.
Kama unadhani staa wa FC Barcelona Lionel Messi anapenda kulinganishwa na staa wa Real Madrid Cristiano Ronaldo basi sikia hii!!
Mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Murgentina Lionel Messi amesema kuwa hataki kulinganishwa na mpinzani wake wa karibu Mreno Cristiano Ronaldo ama mchezaji mwingine yoyote yule.
Messi, 28,ambaye mwaka jana alishinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa kuwabwaga Cristiano Ronaldo na Neymar Jr ameweka wazi kuwa havutiwi kabisa na mjadala unaoendelea duniani kote juu ya nani ni bora kati yake na Ronaldo na kusisitiza kuwa akili yake yote iko kwenye soka lake.
Akiongea na kituo cha luninga cha Misri cha MBC na kuripotiwa na Sports,Messi amesema vyombo vya habari vimekuwa vinapenda kulinganisha vitu.Amesema
"Sijilinganishi na Ronaldo ama mchezaji yoyote yule.Najifikiria mimi,wachezaji wenzangu na jinsi ya kuisaidia FC Barcelona ishinde michezo yake.
ANASEMAJE KUHUSU REAL MADRID!?
Messi ambaye wiki ijayo ataiongoza FC Barcelona kuivaa Real Madrid ya Cristiano Ronaldo amesema kushinda taji la La Liga daima huwa ni ngumu sana hasa kama unapambana na timu kama Real Madrid.
Amesema"Real Madrid ni timu bora duniani,ina wachezaji wazuri sana.Ni washindani wagumu sana,huwa wanatupa shida sana kupata ushindi dhidi yao.
0 comments:
Post a Comment