728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, March 25, 2016

    JOHN OBI MIKEL AULA NIGERIA

    Lagos,Nigeria.

    Kiungo wa Chelsea John Obi Mikel ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles ambayo jioni ya leo itashuka katika dimba la Ahmadu Bello huko Kaduna kuvaana na Misri katika muendelezo wa michezo ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON itakayopigwa 2017 nchini Gabon.

    Mikel,27 amechukua nafasi hiyo kutoka kwa Ahmed Musa wa CSKA Moscow ambaye naye alimbadili nahodha wa siku nyingi Vincent Enyeama aliyejiondoa kufuatia kuwa na msuguano na aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Sunday Oliseh.

    Mikel ambaye alianza kuichezea Nigeria mwaka 2006 wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 pekee amepewa heshima hiyo kutokana na kuwa ni mchezaji mkongwe zaidi katika kikosi cha sasa cha Nigeria kilichojaa sura nyingi ngeni.

    Mpaka sasa Mikel ameichezea Nigeria jumla ya michezo 72 huku mchezo wa leo dhidi ya Misri ukiwa ni mchezo wake wa kwanza akiwa kama nahodha.



     
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: JOHN OBI MIKEL AULA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top