KAZI IPO!!Hii ndiyo kauli rahisi zaidi unayoweza kuitumia kuelezea mpango wa vilabu sita tajiri Ulaya dhidi ya mlinzi wa kulia wa Arsenal Muhispania Hector Bellerin,21.
Taarifa kutoka vyombo vya habari vya Hispania na kuthibitishwa na gazeti la Mundo Deportivo la leo jumatano zinasema kuwa Bellerin aliyejiunga na Arsenal mwaka 2011 akitokea FC Barcelona anawindwa na vilabu sita na tayari vimeshaanza kufanya mipango ya kumng'oa Emirates mwishoni mwa msimu huu.
Mundo Deportivo limevitaja vilabu hivyo kuwa ni FC Barcelona inayomuona Bellerin kama mbadala sahihi wa mlinzi wake Dani Alves anayejiandaa kutimkia China kujiunga na Guanzou Evergrande.
Vilabu vingine vinavyotajwa kumuwania mlinzi huyo wa kulia mwenye uwezo mkubwa wa kushambulia ni pamoja na Bayern Munich,Paris Saint-Germain,Manchester United,Manchester City na
Chelsea.
Mkataba wa Bellerin katika klabu ya Arsenal utafika ukingoni mwaka 2019 hivyo ni jambo la jambo la kukaa na kusubiri kama mlinzi Muhispania atatimka Arsenal.
0 comments:
Post a Comment