728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 31, 2016

    WAKALA:KLABU ZOTE ENGLAND ZINAMTAKA ZLATAN IBRAHIMOVIC ISIPOKUWA MOJA TU


    Paris,Ufaransa.

    Wakala wa mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic,Mino Raiola amesema vilabu vyote vikubwa vya England vimeonyesha nia ya kumtaka mteja wake isipokuwa Manchester City peke yake.

    Raiola amefichua kuwa Manchester City haipo katika mbio hizo kwa sababu msimu ujao itakuwa ikinolewa na Pep Guardiola ambaye ni adui mkubwa wa mteja wake.

    Mbali ya England Raiola ameongeza kuwa vilabu vya Italia pia vinamtaka Ibrahimovic huku akiitaja Inter Milan kama mfano. 

    Wakati huohuo Raiola amesema klabu itakayomsajili Zlatan Ibrahimovic,34 itakuwa imelamba bingo kwani mchezaji huyo bado ana nguvu ya kuendelea kucheza hata kwa miaka mitano zaidi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WAKALA:KLABU ZOTE ENGLAND ZINAMTAKA ZLATAN IBRAHIMOVIC ISIPOKUWA MOJA TU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top