Kigali,Rwanda.
Rwanda imelipa kisasi cha kufungwa na Mauritius baada ya leo jioni kuichapa magoli 5-0 katika mchezo wa kundi H wa kufuzu michuano ya Afcon.
Rwanda ikicheza katika dimba lake la nyumbani la Amahoro imepata magoli hayo kipitia kwa Dominique Nshuti aliyefunga mara mbili,Ernest Sugira,Fibna Omborenga na Jean Baptiste Muriganeza.Rwanda ilichapea goli 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa jumamosi.
Kufuatia ushindi huo Rwanda imefikisha pointi sita na kushika nafasi ya pili ikiwa nyuma ya vinara Ghana wenye pointi nane.
Kikosi cha Rwanda kilichoshuka dimbani leo:
Ndayishimiye,Omborenga,
Bayisenge,Rwatubyaye,
Sibomana,Mukunzi,
Nshimiyimana (Mugiraneza
46'),Nshuti,Iranzi (Hakizimana 46'),Niyonzima (Rushenguziminega ),Sugira.
0 comments:
Post a Comment