Na Paul Manjale.
Paris,Ufaransa.
Miamba ya Ufaransa Paris St-Germain imejipanga kutoa kitita cha £50m kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji hatari wa Liverpool Daniel Sturridge.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la Uingereza ni kwamba kocha wa Paris St-Germain Laurent Blanc ni shabiki mkubwa wa Sturridge,26 na anamuona kuwa ni mbadala sahihi wa nahodha Zlatan Ibrahimovic ambaye ataachana na miamba hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Na katika kuonyesha kuwa kuwa haitanii Paris St-Germain imepanga kutuma wawakilishi wake kwenda nchini Uingereza kumtazama Sturridge wakati atakapokuwa akiichezea Uingereza mchezo wa kirafiki dhidi ya Uholanzi siku ya jumanne.
Inadaiwa Sturridge hana furaha ndani ya Liverpool hasa baada ya kocha Jurgen Klopp kuongea vibaya kuhusu majeraha yake ya mara kwa mara hivyo anaweza kutumia mwanya huo kutimka zake.
0 comments:
Post a Comment