728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 31, 2016

    VIATU VYA MESSI VYAZUA BALAA MISRI

    Cairo,Misri.

    Lionel Messi ameingia matatani baada ya viatu vyake alivyovitoa huko Misri kwa ajili ya kupigwa mnada kutafsiriwa kuwa ni tusi na udharirishaji mkubwa.

    Ikumbukwe katika nchi za kiarabu kumpa/kumtupia mtu viatu hutafsiriwa kuwa ni tusi kwani viatu hukanyaga kila aina ya uchafu.

    Akifanya mahojiano na luninga ya Misri iitwayo MBC Masr katika kipindi maarufu cha "Yes I am Famous"Messi aliombwa na mtangazaji wa kipindi hicho Mona El-Sharkawy achangie kitu chochote ambacho kitauzwa na pesa itayopatikana itatolewa kama msaada kwa watu wa Misri.

    Messi bila kujua kama anafanya kosa alimkabidhi Mona jozi moja ya viatu vyake vya kuchezea mpira na hapo ndipo balaa lilipoanza.

    Azmy Megahed msemaji wa chama cha soka cha Misri amenukuliwa akisema 

    "Kama alinuia kutudharirisha sisi nasema ni bora angejitishwa viatu hivyo kichwani kwake na vichwani mwa watu wote wanaomuuanga mkono.

    "Hatutaki viatu vyake wala hatutaki msaada wowote toka kwa Wayahudi au watu wa Israel.Aende akawape ndugu zake,Argentina imejaa umasikini wa kutupa.

    Naye Mbunge mmoja katika Serikali ya Misri aitwaye Said Hasasin akitumia kipindi chake binasi cha luninga kinachorushwa na Al-Asimah amesema 

    "Hatujawahi kudharirishwa kiasi hiki katika kipindi chote cha miaka 7,000 ya Ustaarabu wetu.Nitakupiga na kiatu changu,Messi.Hiki ni kiatu changu haya kakitoe msaada kwenu Argentina."

    Wamisri tuko milioni 90, tuna heshima zetu.Tuna viatu, hatuli kwa pesa za viatu vya watu.Hivi unajua kuwa Kucha moja ya mtoto wa Kimisri ina thamani kuliko kiatu chako?.Ningekuelewa kama ungetoa jezi,hiyo ina kubalika lakini kiatu??Umetutukana.

    Chini Hasasin akijibu mapigo

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VIATU VYA MESSI VYAZUA BALAA MISRI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top