N'Djaména,Chad.
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ikiwa ugenini N'Djaména imeibanjua timu ya taifa ya Chad kwa bao 1-0 katika mchezo mkali wa kundi G wa kusaka tiketi ya kucheza michuano ijayo ya mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON.
Stars ikicheza katika dimba la ugenini la Stade Omnisports Idriss Mahamat Ouya huko N'Djaména iliwabana vizuri wenyeji Chad na kufanikiwa kupata bao la ushindi dakika ya 30 ya mchezo kupitia kwa nahodha wake Mbwana Samatta.
Kufuatia ushindi huo Stars imefikisha pointi 4 na kuendelea kushika nafasi ya 3 nyuma ya Misri yenye pointi 6 na Nigeria yenye Pointi 4.Misri na Nigeria zitavaana siku ya ijumaa huko Kaduna,Nigeria kugombea uongozi wa Kundi G.
Stars na Chad zitarudiana tena siku ya Jumatatu Machi 28 jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment