Manchester,Uingereza.
Wakala wa Yaya Toure amefichua kuwa yuko katika mazungumzo na vilabu vitatu vikubwa barani Ulaya kwa ajili ya kumhamisha mteja wake katika majira yajayo ya kiangazi.
Wakala huyo aitwaye Dimitry Seluk amevitaja vilabu hivyo kuwa ni Bayern Munich, Juventus na Paris Saint-Germain.
Akiongea na The Sun,Seluk amedai Manchester City haionyeshi dalili ya kuendelea kumuhitaji Toure,32.Mkataba wake umebakisha miezi 12 uishe lakini bado Manchester City wako kimya kana kwamba hakuna jema walilopata toka kwa mteja wake huyo.
Kingine kinachodaiwa kumfanya Toure afikirie kuachana na Manchester City ni ujio wa kocha Pep Guardiola klabuni hapo kwani wawili hao wanadaiwa kutokuwa na mahusiano mazuri tangu wakiwa pamoja FC Barcelona.
0 comments:
Post a Comment