Na Paul Manjale
Kaduna,Nigeria.
Nyota wa Nigeria wanaocheza katika ligi kuu ya Uingereza John Obinna Mikel na Odion Ighalo jana jumamosi walikuwa ni sehemu ya nyota wa Nigeria waliondoka na tuzo katika sherehe ya utoaji tuzo kwa nyota waliofanya vizuri katika soka.
Mikel pamoja na Rais wa NFF Pinnick na nyota wa zamani wa Nigeria Olusegun Odegbami walitwaa tuzo ya Sam Okwaraji Award kwa utumishi wao mwema kwa timu ya taifa huku Ighalo yeye akitwaa tuzo ya mshambuliaji bora wa mwaka na Mfalme wa dimba (King of the Pitch).Kwa upande wa akina mama tuzo ilikwenda kwa Asisat Oshoala
Tuzo zote ni kama ifuatavyo....
Kipa bora la mwaka:Ikechukwu Ezenwa-Sunshine Stars FC
Mlinzi bora wa mwaka:Chinedu Udoji-Enyimba FC
Kiungo bora wa mwaka: Paul Onobi-Sunshine Stars FC
Mshambuliaji bora wa mwaka:Odion Ighalo-Watford FC
Mchezaji mwenye thamani wa ligi ya ndani kwa wanaume (Most Valuable Player (Men) in the NPFL):Gbolahan Salami -Warri Wolves FC
Mchezaji mwenye thamani wa ligi ya ndani kwa wanawake:Most Valuable Player (Women) in the NPFL
Ngozi Ebere-Rivers Angels FC
Klabu/Timu bora ya mwaka
Enyimba FC - Klabu bora ya mwaka
Timu ya taifa ya vijana ya Nigeia ya U-17 (Golden Eaglet)
Kocha bora wa mwaka:Emmanuel Amuneke (U-17 Golden Eaglets)
Kocha bora wa klabu:Kadiri Ikhana-Enyimba FC
Mwamuzi bora wa mwaka:Ferdinand Udoh
Wakala bora wa mwaka wa wachezaji:John Olatunji Shittu
0 comments:
Post a Comment