London,England.
Arsenal imeendelea kuchechemea katika mbio zake za kuusaka ubingwa wa ligi kuu England baada ya leo kupokea kichapo cha mabao 2-1 ikiwa nyumbani Emirates toka Swansea City.
Arsenal ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 15 kupitia kwa Joel Campbell.Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha Swansea City ambayo ilikuja juu na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 32 kupitia kwa Wayne Routridge kabla ya kuongeza bao la pili dakika ya 74 kupitia kwa nahodha wake Ashley Williams kufuatia mlinda mlango Peter Cech kushindwa kuucheza mpira wa adhabu uliopigwa langoni mwake.
Huko Anfield wenyeji Liverpool wamepambana kiume na kufanikiwa.kuitandika Manchester City kwa mabao 3-0.Mabao ya Liverpool yamefungwa na Adam Lallana,James Milner na Roberto Firmino.
Huko Old Trafford wenyeji Manchester United wameendelea kutamba baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wageni Watford.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa kwa mpira wa adhabu na Juan Mata dakika ya 83 ya mchezo.
Matokeo Mengine
Westham United 1-0 Tottenham Hotspurs
Stoke 1-0 Newcastle United
0 comments:
Post a Comment