728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 31, 2016

    YANGA,AZAM ZAPETA KOMBE LA SHIRIKISHO KAZI YABAKI KWA MNYAMA

    Dar es salaam,Tanzania.

    Yanga na Azam zimetinga nusu fainali ya kombe la shirikisho (FA CUP) baada ya leo jioni kushinda michezo yao ya robo fainali.

    Yanga ikiwa nyumbani Uwanja wa Taifa imeitambia Ndanda kwa kuichapa magoli 2-1.Goli la kwanza la Yanga limefungwa na Paul Nonga dakika ya 31 huku la pili likitiwa kimiani kwa mkwaju wa penati na Kelvin Yondani.Goli la Ndanda limefungwa na Kiggi Makasy.

    Katika mchezo mwingine uliopigwa Chamazi Azam imeibuka na ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Prisons.

    Magoli ya Azam yamefungwa na Shomari Kapombe dakika za 9 na 60 na Mcha Hamisi dakika ya 86.Goli la Prison limefungwa na Jeremia dakika ya 31.

    Mchezo wa mwisho wa kombe la shirikisho utapigwa April 9 Simba itakuwa Uwanja wa taifa kuikaribisha Coastal Union ya Tanga.

    Mpaka sasa timu zilizofanikiwa kutinga nusu fainali ni Mwadau,Azam na Yanga.Bingwa wa michuano hii atapata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la shirikisho Afrika.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA,AZAM ZAPETA KOMBE LA SHIRIKISHO KAZI YABAKI KWA MNYAMA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top