Real Madrid imeendelea kuonyesha kuwa siyo mali kitu mbele ya Barcelona baada ya leo timu yake ya vijana kukubali kichapo cha mabao 2-0 katika mchezo wa fainali wa michuano ya Mediterranean International Cup.
Katika mchezo huo uliopewa jina la Mini-Clasico [El Clasico Ndogo] Barcelona ilijihakikishia ushindi kwa magoli ya kipindi cha pili ya Marc Jurado na Toni Caravaca aliyefunga kwa mkwaju wa faulo wa umbali wa mita 30.
Kwa matokeo hayo Barcelona wamekabidhiwa ubingwa wa michuano ya Mediterranean International Cup ambayo hushirikisha timu za watoto za vilabu mbali mbali.
0 comments:
Post a Comment