728x90 AdSpace

Friday, March 25, 2016

THEO WALCOTT KIMEO TENA AUMIA MAZOEZI KUIKOSA UJERUMANI WIKENDI HII

London,England.

Timu ya taifa ya Uingereza imepata pigo baada ya winga wake mwenye kasi kubwa Theo Walcott kupata majeraha ya mguu wakati akifanya mazoezi katika kambi ya timu hiyo inayojiwinda na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ujerumani wikendi hii.

Walcott,27 ambaye kuitwa kwake kwenye kikosi hicho kuliibua maswali mengi vichwani mwa mashabiki wa Uingereza kutokana na kutokuwa katika kiwango bora cha uchezaji ameondolewa na kocha Roy Hodgson katika orodha ya wachezaji watakaosafiri kwenda Berlin kuivaa Ujerumani.

Taarifa za kuumia kwa Walcott zimeongeza maumivu kwa kocha Roy Hodgson ambaye tayari alikuwa amewapoteza kwa majeruhi nyota wengine watatu Ryan Bertrand, Joe Hart na Raheem Sterling.





  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: THEO WALCOTT KIMEO TENA AUMIA MAZOEZI KUIKOSA UJERUMANI WIKENDI HII Rating: 5 Reviewed By: Unknown