Kaduna,Nigeria.
Nigeria imeshindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Misri katika mchezo mkali wa kundi G wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON itakayopigwa Gabon mwakani.
Nigeria ikicheza mbele ya mashabiki wake huko Ahmadu Bello,Kaduna ilifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 60 kupitia kwa Oghenekaro Etebo.
Kuingia kwa bao hilo hakukuwavunja nguvu wageni Misri kwani dakika ya 90 winga Mohamed Salah aliwapatia bao la kusawazisha baada ya kumegewa pande zuri na Ramadan Sobhy.
Kufuatia matokeo hayo Misri bado iko kileleni mwa kundi G baada ya kufikisha pointi 7,nafasi ya pili inashikiliwa na Nigeria yenye pointi 5 huku Tanzania ikiwa na pointi 4 katika nafasi ya 3 huku Chad ikiwa haina pointi hata moja.
Nigeria na Misri zitarudiana tena Machi 29 huko Alexandria,Misri.
Vikosi
Misri IX
Ahmed El-Shennawy; Omar Gaber,Rami Rabia, Ahmed Hegazy, Hamada Tolba; Mohamed Elneny , Ibrahim Salah,Abdallah El-Said;Trezeguet, Koka,Mohamed Salah.
Nigeria XI: Ikeme; Amuzie, Ambrose,Oboabona, Shehu Abdullahi; Mikel, Etebo,Iheanacho; Simon, Musa,Ighalo.
0 comments:
Post a Comment