Na Paul Manjale.
Mauritius.
Timu ya taifa ya Rwanda "Amavubi" leo imekubali kichapo cha bao 1-0 toka kwa timu ya taifa ya Mauritius katika muendelezo wa michezo ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ijayo ya AFCON.
Mauritius ikiwa katika dimba lake la nyumbani la Stade Anjalay, Belle Vue Maurel iliibana vizuri Rwanda na kufanikiwa kupata bao la ushindi dakika ya 59 kupitia kwa Francis Rasolofonirina.
Kufuatia matokeo hayo Mauritius imefanikiwa kushika nafasi ya pili nyuma ya Ghana inayoongoza msimamo wa kundi H.
Rwanda na Mauritius zitarudiana tena siku ya jumanne huko Kigali,Rwanda.
0 comments:
Post a Comment