Yaunde,Cameroon.
Cameroon imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wa Stade Municipal de Limbé baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Afrika Kusini "Bafana Bafana" katika mchezo mkali wa Kundi F wa kufuzu michuano ya AFCON.
Magoli ya Camoroon yamepatikana dakika za 45’ na 67' kupitia kwa Sebastien Siani na mlinzi Nicolas N'Koulou aliyefunga kwa kichwa.
Wageni Bafana Bafana wamepata magoli yao dakika za 17’ na 50 kupitia kwa Tokelo Rantie na Hlompho Kekana.
Cameroon na Bafana Bafana zitarudiana tena siku jumanne jijini Durban.
Vikosi
Bafana Bafana: Khune, Ngcongca ( Coetzee 45’),
Hlatshwayo, Mathoho, Matlaba, Jali, Kekana,
Masango, Makola ( Twala 72’), Rantie,Gabuza ( Serero 46’)
Cameroon: Ndy Assembe, Nkoulou, Chedjou,
Bedimo, Nyom, Mbia, Siani (Matip 78’),Mandjeck, Zoua, Bekamenga, Salli ( Abang 59’)
0 comments:
Post a Comment