Kampala,Uganda.
Goli kipa wa zamani wa Simba SC na timu ya taifa ya Uganda Abel Dhaira amefariki dunia leo jumapili kwa ugonjwa wa Kansa ya utumbo.
Dhaira,28 aliyekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya chuo kikuu cha Iceland kwa gharama za klabu yake ya IBV Vestmannaeyjar amefariki baada ya kuugua kwa miezi kadhaa.
Dhaira aligundulika kuwa na Kansa mwaka jana baada ya awali kudhaniwa kuwa ni Ulcers.
Dhaira alianza safari yake ya kucheza kandanda kwa kuichezea Walukuba Red Stars ya nyumbani kwao Walukuba,Jinja kama mshambuliaji kabla ya kujiunga na Boca Juniors, Wama FC na kisha Aldinah FC.
Baadae Dhaira alianza kudaka akiwa na Mbale
Industrial kabla ya mwaka 2006 kunyakuliwa na Express FC ambayo aliichezea kwa misimu miwili.
Mwaka 2008 Dhaira alijiunga na URA FC na kudumu nayo mpaka mwaka 2010 kabla ya kutua AS Vita ya Congo ambayo hakudumu nayo sana alienda kucheza soka la kulipwa nchini Iceland katika klabu ya IBV Vestmannaeyjar.Hiyo ikiwa ni mwaka 2011-2012 kabla ya kutua Simba.
Baada ya mambo kumuendea kombo ndani ya Simba,Dhaira alirejea tena Iceland na kujiunga na IBV Vestmannaeyjar ambayo alikuwa akiichezea mpaka umauti unamfika.
0 comments:
Post a Comment