Alexandria,Misri.
Nigeria imeshindwa kufuzu michuano ya AFCON kwa mara ya pili mfululizo baada ya jana usiku kufungwa bao 1-0 na Misri katika mchezo mkali wa kundi G uliopigwa katika uwanja wa Borg El-Arab huko Alexandria.
Bao lililofifisha matumaini ya Nigeria kwenda Gabon mwakani limefungwa dakika ya 68 na kinda Ramadan Sobhy anayekipiga katika klabu ya Al Ahly.
Sobhy aliyekuwa ameingia uwanjani akitokea benchi alifunga bao hilo baada ya shuti lake kumgonga Mlinzi wa Nigeria Shehu Abdullahi na kumpoteza maboya mlinda mlango Daniel Akpeyi.
Kufuatia matokeo hayo Misri iko kileleni mwa Kundi G baada ya kufikisha alama saba,Nigeria iko nafasi ya pili na alama zake mbili huku Tanzania ikiburuza mkia baada ya kuwa na alama moja pekee.
Hivyo kimahesabu Misri ni kama tayari imeshafuzu kwani kati ya Tanzania ama Nigeria hakuna timu itakayofikia alama za Misri.
Wakati huohuo Morocco imekuwa taifa la kwanza kufuzu michuano ya Afcon ikitokea Kundi F baada ya kuibanjua Cape Verde 2-0 huko Marrakech.Magoli yote ya Misri yametiwa kimiani na straika Youssef El Arabi.
0 comments:
Post a Comment