Na Paul Manjale
Milan,Italia.
Manchester United imeripotiwa kujianda kumtwaa mlinzi mahiri wa Inter Milan ya Italia Mcolombia Jeison Murillo kwa ajili ya kuimarisha safu yake ya ulinzi ambayo msimu huu imekuwa ovyo.
Kutoka gazeti la The Mirror la Uingereza taarifa zinadai kuwa Manchester United inamuona Murillo,23 kuwa ndiye mtu sahihi wa kuleta uimara katika safu yake ya ulinzi ambayo imekuwa ikimtegemea zaidi Chris Smalling.
Murillo aliyefanya vyema mwaka jana akiwa na kikosi cha Colombia katika Copa America huko Chile na kutangazwa mchezaji bora kijana wa michuano hiyo anakadiriwa kuwa na thamani ya £15m.
Msimu huu Murillo ameicheza Inter Milan jumla ya michezo 27 huku akiifungia mabao mawili.
0 comments:
Post a Comment