London,England.
Nyota wa zamani wa England na Liverpool Emile
Heskey amesema straika wa Tottenham Hotspur Harry Kane ana sifa za kuchezea Real Madrid.
Akiongea na Daily Mail, Heskey amesema Kane,22 ana sifa zote za kumfanya aweze kuchezea vilabu vikubwa duniani na kuongeza kuwa nyota huyo wa England ni bora kama alivyo Karim Benzema katika klabu ya Real Madrid.
Msimu huu Kane amefunga magoli 25 na kuiweka Tottenham Hotspur katika mbio za kuwania taji la ligi kuu England.Msimu uliopita Kane alifunga magoli 31 katika michuano yote.
Mbali ya Kane,Heskey pia amewataja nyota wengine wa England Dele Alli na Jamie Vardy kuwa ni moto wa kuotea mbali na wana sifa za kuchezea vilabu vikubwa.
0 comments:
Post a Comment