Manchester,England.
Kocha Manuel Pellegrini amedokeza kuwa atapendelea kubaki England hata baada ya kuachana na Manchester City mwishoni mwa msimu huu.
Pellegrini,62 ambaye ataiacha Manchester City mikononi mwa Pep Guardiola hivi karibuni amedokeza kuwa England bado ni mahali sahihi kwa yeye kufanya kazi kama kocha.
Licha ya kuhusishwa kujiunga na vilabu vya Valencia na Zenit St. Petersburg bado Pellegrini ameoneka kuwa mzito kuondoka England na amesisitiza kuwa akipata timu yoyote yenye project nzuri hatasita kujiunga nayo hata kama haishiriki michuano yoyote ile ya Ulaya.
Akiongea na Telegraph Pellegrini amesema vilabu vya England vina mazingira mazuri ya kufanyia kazi,pesa nyingi na mipango mikubwa.Hata ukiwa kocha wa vilabu vidogo bado una nafasi ya kusajili wachezaji wazuri kwani pesa ipo.
0 comments:
Post a Comment