Suarez akiwa na Oscar Tabarez
Montevideo, Uruguay.
Kama ilivyo desturi kuwa kila mnyonge ana mnyonge wake basi hata kila bosi ana bosi wake.
Kauli hiyo imejidhihirisha hivi majuzi baada ya mshambuliaji hatari wa FC Barcelona na Uruguay Luis Suarez kukiri kuwa Sergio Ramos [Real Madrid/Hispania],Thiago Silva [PSG/Brazil] na Diego Godin [Atl Madrid/Uruguay] ndiyo walinzi wagumu zaidi aliowahi kukutana nao katika maisha yake ya soka.
Licha ya kucheza Uholanzi na Uingereza kwa kipindi kirefu Suarez hadhani huko kote kama kuna walinzi nuksi kama hao aliowataja hapo juu kwani wamekuwa wakimpa wakati mgumu sana pindi anapokutana nao katika michezo mbalimbali.
Wakati huohuo Suarez amewataja Martin Lasarte na Oscar Tabarez kuwa ndiyo makocha wawili anaowahusudu zaidi huku akiwatupilia mbali Brendan Rodgers na Luis Enrique.
Chini ya Lasarte,Suarez alishinda taji la ligi kuu ya Uruguay mwaka 2006 akiwa na klabu ya Nacional akifunga mabao 10 katika michezo 27.
Tabarez alimwita Suarez kuichezea Uruguay kwa mara ya kwanza mwaka 2007 na miaka minne baada wakashinda ubingwa wa Copa Amerika.
Chini Thiago Silva mmoja kati ya walinzi nuksi kwa mujibu wa Suarez
0 comments:
Post a Comment