Berlin,Ujerumani.
Mlinda mlango Manuel Neuer amejiondoa katika kikosi cha Ujerumani ambacho usiku wa leo kitashuka dimbani kuvaana na Italia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Kwa mujibu wa chama cha soka cha Ujerumani DFB ni kuwa Neuer,30 amejiondoni kikosini kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya tumbo.
Kutokana na kumkosa Neuer Kocha wa Ujerumani Joachim Low atalazimika kuwategemea walinda mlango Bernd Leno,Kevin Trapp na Marc-Andre ter Stegen kusaka ushindi dhidi ya Italia leo baada ya siku ya jumamosi kupachwa 3-2 na England.
0 comments:
Post a Comment