Saint-Denis,Ufaransa.
Ufaransa imeshinda mchezo wake wa kwanza tangu tangu ilipokumbwa na shambulio la ugaidi Novemba 13 mwaka jana baada ya jumanne usiku kuitandika Urusi kwa mabao 4-2 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa huko Stade de France,Saint-Denis.
Magoli yaliyoipa Ufaransa ushindi huo mnono yamefungwa na N’Golo Kante (8'),Andre-Pierre Gignac (38),Dimitri Payet (64) na Kinglsey Coman (76) huku yale ya Urusi yakifungwa na Alexander Kokorin (56 '), na Yuri Zhirkov ( 68' )
Katika mchezo mwingine Ureno ikiwa nyumbani imeitambia Ubelgiji baada ya kuichapa magoli 2-1 kwa magoli ya Cristiano Ronaldo na Luis Nani huku Romelo Lukaku akiifungia Ubelgiji goli la kufutia machozi akiunganisha pasi safi ya kaka yake Jordan Lukaku.
0 comments:
Post a Comment