728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 01, 2016

    FIFA YAMFUNGIA MWAKA MMOJA EMMANUEL EBOUE

    Sunderland,England.

    Shirikisho la vyama vya soka duniani FIFA limemfungia mwaka mmoja mlinzi Emmanuel Eboue 32 kwa kosa la kushindwa kulipa deni la siku nyingi analodaiwa na wakala wake wa zamani Sebastien Boisseau.

    Fifa imefikia hatua hiyo baada ya kamati ya nidhamu ya shirikisho hilo CAS kuutupilia mbali utetezi wa mlinzi huyo wa zamani wa Arsenal na Ivory Coast.

    Julai mwaka 2013 FIFA ilimuagiza Eboue kumlipa Boisseau kiasi chote anachodaiwa lakini mlinzi huyo hakutimiza agizo hilo hali iliyofanya alimwe faini ya £21,000 huku akipewa onyo la kukumbana na adhabu kali.

    Wakati huohuo Sunderland imetangaza kumtema Eboue zikiwa ni siku 12 zimepita tangu imsajili akiwa kama mchezaji huru baada ya kutemwa na Galatasaray.

    Kupitia tovuti yake Sunderland imesema imefikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na FIFA na kuongeza kuwa Eboue hakusema kama ana kesi FIFA.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FIFA YAMFUNGIA MWAKA MMOJA EMMANUEL EBOUE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top