728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 01, 2016

    MASHABIKI UFARANSA WATAJA KOSI LAO LA EURO 2016,WAWAKATAA SCHNEIDERLIN,MANGALA

    Paris,Ufaransa.

    Michuano ya Euro ikiwa imebakiza miezi miwili ianze kutimua vumbi lake nchi Ufaransa mashabiki wa soka wa nchi hiyo wamemrahisishia kazi kocha wao Didier Deschamps baada ya kutaja kikosi cha wachezaji 23 wachotaka kiiwakilishe nchi yao katika michuano ijayo ya Euro 2016 ambao wao ni wenyeji.
      
    Mashabiki hao ambao waliombwa na mtandao wa L’Equipe kutoa mapendekezo juu ya wachezaji gani wanafaa kuunda timu yao ya taifa wamewajumuisha kikosini nyota kama Paul Pogba na Patrice Evra huku kukiwa hakuna nafasi kwa kiungo wa Manchester United Morgan Schneiderlin na mlinzi wa Eliaquim Mangala.

    Baadhi ya wachezaji waliopendekezwa kuunda kikosi hicho ni:

    Hugo Lloris (Tottenham),Laurent Koscielny na Olivier Giroud (Arsenal),Mamadou Sakho (Liverpool),Bacary Sagna (Manchester City),
    Moussa Sissoko (Newcastle United).

    Wengine ni Ng'olo Kante (Leceister City),Dimitri Payet (Westham United) na Anthony Martial (Manchester United).

    Michuano ya Euro 2016 itaanza kutimua vumbi lake Juni na kumalizika Julai nchini Ufaransa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MASHABIKI UFARANSA WATAJA KOSI LAO LA EURO 2016,WAWAKATAA SCHNEIDERLIN,MANGALA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top