728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, April 01, 2016

    KUZIONA SERENGETI BOYS v THE PHARAOS NI 2000/=

    Dar es salaam,Tanzania.

    Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
    limetangaza kiingilio cha shilingi elfu mbili tu
    (2,000) ndio kitakachotumika katika mchezo wa kesho Jumamosi kati ya Serengeti Boys (Tanzania) v The Pharaohs (Misri) katika
    uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

    TFF imeweka kiingilio cha shilingi elfu mbili tu (2000) uwanja mzima, kutoa nafasi kwa wapenzi wa mpira wa miguu nchini kujitokeza kwa wingi siku ya Jumamosi kuja kushuhudia mchezo huo wa kirafiki wa
    kimataifa kati ya timu za vijana za Tanzania v Misri.

    Serengeti Boys inashuka dimbani kucheza na The Pharaohs mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa kujipima nguvu, ikiwa ni sehemu ya maandalizi na kujiandaa na mchezo wa
    kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi ya Shelisheli Juni – Julai mwaka huu.

    Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utachezeshwa na waamuzi wa kimataifa
    wenye beji za FIFA ambao ni Israel Mjuni,akisaidiwa na Soud Lila, Frank Komba,
    mwamuzi wa akiba Jonesia Rukyaa, huku kamisaa wa mchezo akiwa Isabella Kapera.

    Upande wa kikosi cha timu ya Taifa ya Misri kimewasili nchini jana mchana saa 7:30 mchana kwa shirika la ndege la Ethiopia,kikiwa na msafara wa watu 33 wakiwemo wachezaji 25 na viongozi 8.

    The Pharaohs wanatarajiwa kufanya mazoezi leo jioni saa 10 kamili katika uwanja wa
    Taifa jijini Dar es salaa,baada ya kuwa wamefanya mazoezi jana jioni katika uwanja wa Karume.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUZIONA SERENGETI BOYS v THE PHARAOS NI 2000/= Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top