NAIROBI, Kenya.
MABAO mawili ya kila kipindi ya washambuliaji
Ayub Timbe na Eric Johanna yameipa Harambee Stars ushindi mabao 2-1 nyumbani dhidi ya wageni Congo
Brazzaville katika mchezo mkali wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON
hapo mwakani nchini Gabon.
Katika mchezo huo ulioisha hivi punde katika
uwanja wa Safaricom/Moi Kasarani wageni Congo Brazzaville ndiyo walikuwa wa
kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 19 baada ya nahodha wake Oniangue
kufunga kwa mkwaju wa penati uliopatikana baada ya Ferebory Dore kuangushwa
ndani ya boksi na kiungo wa Kenya Ismail Gonzalez.
Baada ya kuingia kwa bao hilo Kenya iliamka na
kuanza kulisakama lango la Congo Brazzaville na ilipofika dakika ya 27 juhudi
zao zilizaa matunda baada ya Ayub Timbe kufunga bao la kusawazisha baada ya
kuwazidi mbio walinzi wa Congo Brazzaville.Bao la ushindi limefungwa Eric
Johanna dakika ya 61.
Kwa matokeo hayo Guinea Bissau ambayo iliifunga
Kenya nyumbani na ugenini imefuzu fainali zake za kwanza za AFCON baada ya Jana
Jumamosi kuifunga Zambia kwa mabo 3-2 huko
Bissau na kufikisha pointi 10 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile
katika kundi hilo.
0 comments:
Post a Comment