728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, September 13, 2016

    MOURINHO AELEZA KWANINI NI VIGUMU KWA VILABU VYA ENGLAND KUTWAA TAJI LA LIGI YA MABINGWA ULAYA


    Manchester, England.

    WAKATI ligi ya mabingwa barani Ulaya ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi lake leo Jumanne,Kocha wa Manchester United,Mreno Jose Mourinho,amesema ni vigumu sana kwa vilabu vya England kutwaa taji la michuano hiyo kutokana na kubanwa sana na ratiba ya ligi ya primia.

    Mourinho ambaye msimu huu hana chake katika michuano hiyo baada ya msimu uliopita klabu yake ya Manchester United kuangukia katika michuano ya Europa Ligi kufuatia kumaliza nje ya vilabu vinne vya juu amesema mahitaji ya ligi ya primia pamoja na yale ya michuano ya ndani yamekuwa makubwa kiasi cha kuvinyima vilabu shiriki muda wa kupumzika na kujiandaa.

    Mourinho ameliambia Daily Mail kuwa ligi ya primia pamoja na michuano ya ndani (FA Cup na Capital EFL) inavipa vilabu vya England wakati mgumu sana kufanya vizuri katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.


    Amesema "Nchi nyingine zinaijali sana michuano ya ligi ya mabingwa.Zinatoa muda mrefu kwa vilabu vyao kupumzika na kujiandaa lakini katika nchi hii [England] ligi ya primia ndiyo inayopewa kipaumbele cha kwanza.

    Taasisi zinazoongoza michuano hazitoi mapumziko/ulinzi ambao unaweza kuwa na msaada.Masaa 24 zaidi ama 48 zaidi kwa ajili ya kupumzika na kujiandaa.

    Kauli hiyo ya Mourinho imekuja wakati England ikiwa imefikisha miaka minne sasa bila ya kuingiza timu hata moja katika fainali nne zilizopita za klabu bingwa ya Ulaya.

    Msimu huu katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya,England itawakilishwa na vilabu vya Arsenal,Manchester City,Tottenham na mabingwa wa ligi ya primia Leceister City.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MOURINHO AELEZA KWANINI NI VIGUMU KWA VILABU VYA ENGLAND KUTWAA TAJI LA LIGI YA MABINGWA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top