Corsica,Ufaransa.
NYOTA wa kimataifa wa Burkina Faso,BEN Idriss Derme,(pichani) amefariki dunia akiwa uwanjani baada ya kukumbwa la shambulio la moyo.
Derme,34,aliyekuwa akimudu kucheza nafasi ya kiungo mkabaji na beki wa kati amekumbwa na umauti huo jana Jumatatu wakati akiichezea klabu yake ya AJ Biguglia katika mchezo wa kombe la ligi ya Ufaransa dhidi ya Furiani katika uwanja wa Stade Paul-Tamburini.
Ripoti kutoka nchini Ufaransa zinasema Derme alidondoka na kufariki dakika chache baadae licha madaktari waliokuwepo uwanja hapo kujitahidi kuokoa maisha yake.
Kabla ya umauti kumfika Derme aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Burkina Faso michezo minne ya kimataifa pamoja na vilabu vya Etoile Filante,Sheriff Tiraspol,US Ouagadougou USC Corte, CA Bastia na EF Bastia.
0 comments:
Post a Comment