KATIBU
mkuu wa Mbeya City Fc, Emmanuel Kimbe amewataka mashabiki wa timu
hiyo popote walipo duniani
kutokuwa na wasiwasi wowote kuhusu majaaliwa ya kikosi chao msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara, kufuatia kuondoka kwa nyota kadhaa waliokuwa sehemu ya mafanikio kwa misimu miwili iliyopita.
kutokuwa na wasiwasi wowote kuhusu majaaliwa ya kikosi chao msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara, kufuatia kuondoka kwa nyota kadhaa waliokuwa sehemu ya mafanikio kwa misimu miwili iliyopita.
Akizungumza
mapema leo na Tovuti rasmi ya klabu hiyo kwenye ofisi za timu zilizopo
Mkapa Hall, jijini Mbeya, Kimbe alisema kuwa ni wazi kuondoka kwa
nyota hao kumewashtua wengi , lakini kwenye soka mchezaji kuhama timu
moja kwenda nyingine ni jambo la kawaida.
“Tulio
wengi tumeshtuka lakini kwenye soka hili ni jambo la kawaida, zipo
timu zimewahi kuondokewa na wachezaji wengi na baadaye zikafanya vizuri,
kikubwa ni maandalizi ya kikosi kipya ambacho kinakuwa kimeundwa baada
ya walikuwepo kuondoka ” alisema.
Akiendelea
zaidi Katibu Mkuu Kimbe alidokeza kuwa City inayo timu nzuri ya vijana
ambayo imekuwa sehemu ya mafanikio kwasababu wachezaji wote
wanaaopandishwa kutoka kwenye kikosi hicho cha U20 wamekuwa wakifanya
vizuri kwenye timu kubwa.
“Tuna
timu nzuri ya U20, vijana wengi tumekuwa tukiwapandisha kutoka huko na
wamekuwa sehemu ya mafanikio huku juu, mfano mzuri ni Rafael Daud,
alipandishwa wakati wa dirisha dogo, ameonyesha uwezo mkubwa ,
tunatarajia makubwa zaidi msimu mpya kutoka kwake pamoja na wengine
tutakaowapandisha safari hii”.
“Hivyo
basi hakuna haja ya kuwa na hofu kwa mashabiki wa timu yetu, naomba
muamini timu itakuwa vizuri msimu ujao kupitia vijana wetu
tunaowapandisha na pia wazoefu wachache tutakaowasajili kuja kusaidiana
na waliopo. hii ndiyo soka kwa sababu sisi tunaweza kusajili mchezaji
kutoka timu nyingine, ndivyo timu nyingine zinaweza kusajili kutoka
kwetu, hili lisiwatie hofu, City itabaki kuwa City na hilo
halitabadilika, alisema.
Kuhusu
suala la kuisha kwa mikataba ya wachezaji na wengine kuondoka, Kimbe
alisema kuwa ni kweli mikataba ya wachezaji wao wengi ilikuwa inakwisha
baada ya msimu na kulikuwa na mazungumzo kabla na wachache kati yao
walikubali kuongeza mikataba mipya na wengine walikataa.
“Hakukuwa
na namna katika hili, tulizungumza nao mapema lakini waligoma, nadhani
ni kwa sababu walitaka kuwa huru ili wafanye makubalino mapya kule
wanakokwenda, tulijitahidi lakini waligoma kwa sababu tayari kulikuwa na
shinikizo nyuma yao, kama klabu hatukuwa na njia nyingine ya kuwafanya
wabakie, tunawatakia heri huko walikokwenda kwa sababu soka ndivyo
ilivyo”. alimaliza Kimbe.
0 comments:
Post a Comment