728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 21, 2015

    MAVUNO:LIVERPOOL YASAJILI KIFAA KINGINE CHA NGUVU

    LIVERPOOL,ENGLAND


    Klabu ya Liverpool imeendelea kuimarisha kikosi chake hii ni baada ya jumamosi juni 20 kufanikiwa kumsajili kwa mkataba wa
    miaka mitano mlinzi  Joe Gomez kutoka klabu ya Charlton kwa ada ya $7m (£3.5m)

    Gomez 18 ambaye pia ni mchezaji wa kikosi cha (U19) cha England alifanikiwa kuichezea Charlton jumla ya michezo 24 katika msimu ulioisha wa ligi daraja la kwanza nchini England.

    Kutua Liverpool kwa Gomez ambaye anaweza kucheza nafasi nyingi za ulinzi hasa ulinzi wa kati na kushoto kunaashiria mwisho wa uwepo wa mlinzi Sebastian Coates klabuni hapo.

    Gomez anakuwa mchezaji wa nne kutua Liverpool baada ya James Milner,Danny Ings na Adam Bogdan.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAVUNO:LIVERPOOL YASAJILI KIFAA KINGINE CHA NGUVU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top