728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 24, 2015

    USAJILI:LIVERPOOL YAMNASA FIRMINO,WENGER AENDELEA KUICHOKONOA CHELSEA

    Firmino:Klabu ya Liverpool imefanikiwa kuizidi ujanja klabu ya Manchester United baada ya kushinda mbio za kumsajili kiungo mshambuliaji wa klabu ya Hoffenheim Roberto Firmino.Firmino,23 alivumishwa kufikia makubaliano
    ya kujiunga na Manchester United lakini Liverpool imekuja nyuma na kutoa dau la £29m ambalo ni kubwa mara mbili zaidi ya lile la £13m Manchester United.
    Nordfeldt:Klabu ya Swansea City imeendelea kujiimarisha tayari kwa msimu ujao wa ligi baada ya leo hii kuripotiwa kuinasa saini ya mlinda mlango Msweden Kristoffer Nordfeldt 26 toka klabu ya Heerenveen ya Uholanzi.Nordfeldt amesaini mkataba wa miaka mitatu ya kuichezea miamba hiyo ya Wales.Nordfeldt anakuwa mchezaji wa tatu kutua Swansea City baada ya winga Andre Ayew na mlinzi Franck Tabanou.


    Sow:Klabu ya Sunderland imepiga hodi katika klabu ya Fenerbahce ya Uturuki kwa ajili ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa klabu hiyo Msenegal  Moussa Sow.Sow ameifungia  Fenerbahce magoli 15 katika michezo 33 msimu ulioisha.
    Musonda:Klabu ya Arsenal imeendelea kuichokoza klabu ya Chelsea baada ya kuanza kumnyatia kiungo kinda Charly Musonda Jr,18.Arsenal imetenga £8m ili kumsana kinda huyo anayewindwa pia na vilabu vya Marseille na Paris Saint Germain.
    Paulinho:Klabu ya Watford inajipanga kuwavamia wapinzani wao wa jiji la jiji la London klabu ya Tottenham kwa ajili ya kumsajili kiungo wa klabu hiyo aliyefulia Mbrazili Paulinho.
    Tokeo la picha la roberto pereyra juventus
    Pereyra:Klabu ya Juventus imetangaza kumsijili moja kwa moja kiungo  Roberto
    Pereyra toka klabu ya Udinese kwa ada ya 14m (£10m).Juventus imemsajili Pereyra baada ya kuridhishwa na kiwango chake wakati akikitumikia kikosi hicho kwa mkopo.

    Tokeo la picha la mohamed salah
    Salah:Klabu ya Inter Milan imeripotiwa kutaka kumsajili winga wa klabu ya Chelsea  Mohamed Salah ikiwa nyota huyo Mmisri atakataa ofa ya kurudi tena katika klabu ya Fiorentina kwa mkopo.(Daily Mail) 

    Payet:Klabu ya West Ham United  imekubali kutoa  kitita cha £12m kwa ajili ya kumsajili kiungo wa klabu ya Marseille Dimitri.Payet,28.(Daily Mail)




    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:LIVERPOOL YAMNASA FIRMINO,WENGER AENDELEA KUICHOKONOA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top