SIMBA SC imeingia Mkataba wa miaka mwaka mmoja na kocha Dylan Kerr mzaliwa wa Malta na mchezaji wa zamani wa England kwa ajili ya kuinoa
klabu hiyo kuanzia Julai mwaka huu.
Kerr aliyezaliwa Januari 14 mwaka 1967 mjini Valletta amefikia makubaliano ya kuingia Mkataba wa mwaka mmoja na Simba SC wenye kipengele cha kuongezewa mmoja zaidi, iwapo atafanya kazi nzuri.
Kerr anakuja Simba SC akitokea klabu ya Ligi Kuu ya Vietnam, Hai Phong aliyojiunga nayo Januari mwaka 2014.
SOKA LAKE
Kerr amechezea vilabu ya Sheffield Wednesday, Arcadia Shepherds ya Afrika Kusini na Leeds United ya England huku akifanikiwa kuuonja utamu wa ligi kuu ya nchi hiyo kwa kushuka dimbani mara 14 akicheza kama mlinzi wa kushoto.

0 comments:
Post a Comment