Wakazi wa kitongoji duni cha Mathare katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, sasa wanaweza kupata maji safi ya kunywa na kwa
matumizi mengine.
Mpango unaoungwa mkono na serikali umezinduliwa kwenye mji mkuu wa Kenya Nairobi unaowawezesha watu wanaoishi kwenye mitaa ya mabanda kununua maji kwa kutumia kadi.
Vituo vya kuuza maji vimebuniwa kote katika sehemu za mabanda ambapo wenyeji hutumia kadi zilizo na pesa kununua maji safi na kwa bei nafuu.
Wenyeji wa mitaa ya mabanda nchini Kenya wamekuwa na tatizo la kupata maji safi ambapo hulazimika kununua maji kwa bei ghali kutoka kwa wauzaji au kutoka kwa magenge ambayo hudhibiti na kuuza maji hayo kwa kuyachuuza.
Mradi kama huo umefaulu katika baadhi ya maeneo ya vijijini nchini Kenya, lakini hii ni mara ya kwanza kuzinduliwa katika mji huo mkuu.
0 comments:
Post a Comment