Mlinzi na nahodha wa zamani wa Simba, Joseph Owino amejiunga na timu ya Sofapaka inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya.
Mlinzi huyo wa zamani wa SC Villa na URA FC aliichezea Simba kwa vipindi viwili tofauti kabla ya kuamua kuondoka baada ya msimu uliopita kuisha kutokana na kusugua benchi.
Owino ambaye pia aliwahi kuichezea Azam fFC anaungana na Mganda mwenzake, Herman Wasswa ambaye alisaini mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo Ijumaa iliyopita.
Akiwa Sofapaka, beki huyo mganda atakuwa chini ya kocha kutoka nchini kwao, Sam Timbe.
0 comments:
Post a Comment